Manchester City Wahamia kwa Matheus Nunes

Klabu ya Manchester City baada ya kushindwa kumsajili mchezaji wa klabu ya Westham United Lucas Paqueta sasa wamehamia kwa kiungo klabu ya Wolves raia wa Ureno Matheus Nunes.

Manchester City wanataka kuboresha eneo lao la kiungo msimu huu baada ya kuwakosa wachezaji wake kama Ilkay Gundogan aliyetimkia klabu ya Barcelona na Kevin de Bruyne ambaye amepata majeraha yatakayomueka nje kwa kipindi fulani.manchester CityKiungo Matheus Nunes mwenye miaka 24 amekua na kiwango bora sana ndani ya klabu ya Wolves na kua moja ya wachezaji muhimu ndani ya klabu hiyo na kuwavutia Man City kuhitaji huduma yake klabuni hapo.

Mabingwa hao wa soka barani ulaya wanatajwa wanafikiria kutuma ofa yao kwa klabu ya Wolves kwasasa kwajili ya kupata huduma ya Matheus Nunes ambaye yupo kwenye orodha ya juu kabisa ya viungo wanaohitajika klabuni hapo.manchester CityKlabu ya Wolves wao wanaripotiwa hawako tayari kupokea ofa endapo itacheleweshwa klabuni,Hivo kama Manchester City wanahitaji kweli huduma ya kiungo huyo wanapaswa kupeleka ofa mapema ili kuweza kumpata kiungo huyo kwani Wolves wanahitaji ofa mapema ili waweze kutafuta mbadala wa mchezaji huyo.

Acha ujumbe