Klabu ya Manchester City ambao ni mabingwa wa ulaya leo watashuka dimbani katika mchezo wa Uefa Super Cup kumenyana na mabingwa watetezi wa Uefa Europa League klabu ya Sevilla.
Mchezo huu ambao hua unakutanisha mabingwa wa makombe ya ulaya ambayo ni kombe la ligi ya mabingwa ulaya pamoja na kombe la Uefa Europa league ambapo mshindi ananyakua taji hilo linalofahamika kama Uefa Super Cup.Klabu ya Manchester City ilifanikiwa kutwaa taji la ligi ya mabingwa ulaya kwa kuifunga klabu ya Inter Milan ya nchini Italia, Huku leo wakikutana na mabingwa wa muda wote wa ligi ya Uefa Europa League klabu ya Sevilla.
Mchezo wa leo unatarajiwa kua mchezo mkali na wenye ushindani mkubwa kwani vilabu vyote vinavyokutana ni mabingwa wa makombe ya ulaya msimu uliomalizika hivo ni mchezo ambao unatarajiwa kua mgumu kwa timu zote.Klabu ya Manchester City kuelekea mchezo wa leo wa Uefa Super Cup watakwenda wakiwa wana pigo la kumkosa kiungo wao mahiri kwenye klabu hiyo Kevin de Bruyne ambaye atakua nje ya uwanja kwa miezi kadhaa.