UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa nyota wao wote walifanya kazi kubwa dhidi ya watani zao wa jadi Simba na kuongeza kuwa wataendelea kazi hiyo kwenye mashindano mengine.
Ni Maxi Nzengeli na Yao Attohoula hawa walianza kikosi cha kwanza kwenye Kariakoo Dabi fainali ya Ngao ya Jamii, Tanga huku Hafiz Konkoni yeye akitokea benchi.Katika mchezo huo Yanga ilipoteza kwenye changamoto za penalti 1-3 ambazo walipata Simba na kutwaa Ngao ya Jamii 2023 huko Dimba la Mkwakwani, Tanga.
Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa licha ya kushindwa kutwaa taji hilo ambalo walikuwa wanalihitaji wachezaji wao walionyesha uwezo mkubwa.
“Unaona wachezaji wetu walionyesha uwezo mkubwa ikiwa ni pamoja na Maxi Nzengeli, Yao hilo limeonyesha namna ukomavu ulivyo pamoja na kasi iliyopo kwa ajili ya msimu mpya ambao utakuwa na ushindani mkubwa.“Yale yaliyotokea yamepita na sasa tumeona wachezaji walipambana mwanzo mwisho na wapinzani wetu wanajua hilo, bado tuna muda wa kuendelea kufanya vizuri,