Bernardo Silva Kusaini Kandarasi Mpya

Kiungo wa klabu ya Manchester City raia wa kimataifa wa Ureno Bernardo Silva anakaribia kusaini mkataba mpya ndani ya klabu hiyo utaoendelea kumuweka zaidi klabuni hapo.

Bernardo Silva ambaye amekua kwenye mazungumzo ya kuongeza mkataba mpya ndani ya klabu hiyo kwa muda mrefu, Hatimaye mchezaji huyo amekubali kusaini mkataba mpya na mabingwa hao wa Uingereza ambao utamuweka klabuni hapo mpaka mwaka 2026.bernardo silvaKiungo huyo alikua anahitajika na klabu ya Barcelona kwa kipindi kirefu lakini mabingwa hao wa soka nchini Hispania wameshindwa kumshawishi mchezaji huyo kuondoka kwenye viunga vya Etihad na kujiunga nao.

Moja ya sababu ambazo zinaelezwa kuwazuia klabu ya Barcelona kushindwa kupata saini ya kiungo huyo wa kimataifa wa Ureno ni suala la kiuchumi ambalo limekua likiiandama klabu hiyo kwa misimu kadhaa sasa.bernardo silvaKiungo Bernardo Silva ni wazi sasa ataendelea kuitumikia klabu hiyo kwa miaka mingine mitatu baada ya makubaliano ya pande zote mbili, Ambapo klabu hiyo imemuongezea maslahi mchezaji huyo na kumshawishi mchezaji huyo kusalia kikosini.

Acha ujumbe