Kiungo wa klabu ya Manchester City na timu ya taifa ya Ureno Bernardo Silva anaelezwa kukaribia kujiunga na klabu ya Barcelona mabingwa wa soka nchini Hispania.
Bernardo Silva ameonesha nia ya kutimka ndani ya klabu ya Manchester kwa muda mrefu sasa, Lakini klabu hiyo ilitumia nguvu kumbakiza msimu huu inaonekana kuna kila namna mchezaji huyo atatimka ndani ya klabu hiyo.Baada ya kauli ya klabu ya Man City Pep Guardiola alipoulizwa kuhusu kiungo huyo kujiunga Barca ambapo alisema “Sihitaji mchezaji ambaye hataki kuwepo hapa lakini hatujapata ofa sahihi mpaka sasa na kama wanamuhitaji mchezaji huyo waje walete ofa sahihi klabuni kwetu”
Kiungo huyo wa kimataifa wa Ureno amekua moja ya wachezaji muhimu ndani ya klabu hiyo tangu alipojiunga na timu hiyo akitokea Monaco mwaka 2017 hatimae anakaribia kutimka ndani ya klabu hiyo.Kiungo Bernardo Silva kama atafanikiwa kuondoka ndani ya City na kujiunga na Barcelona atakua hana deni ndani ya timu hiyo, kwani atakua ameshinda kila kitu ndani ya klabu hiyo kama taji la ligi kuu ya Uingereza, Fa Cup, Carabao Cup, na taji la ligi ya mabingwa ulaya.