Nottingham Forest Yamuibukia Kipa Arsenal

Klabu ya Nottingham Forest imepanga kumsajili golikipa mbadala wa klabu ya Arsenal raia wa kimataifa wa Marekani Matt Turner ambapo mpaka sasa mazungumzo yanaenda vizuri.

Nottingham Forest wamefikia hatua nzuri kwenye mazungumzo na klabu ya Arsenal na wanataka kuhakikisha dili hilo linakamilika mapema kabla ya msimu mpya kuanza mapema wiki ijayo.Nottingham ForestKlabu ya Arsenal kwasasa nao wamefikia hatua nzuri katika kuinasa saini ya golikipa wa Brentford David Raya, hivo itakua rahisi kwa klabu hiyo kukubali kumuachia golikipa huyo ambaye alikua chaguo la pili klabuni hapo.

Matt Turner ni golikipa mzuri na hilo amekua akilidhihirisha mara kwa mara anapokua anapewa nafasi klabuni hapo, Hivo klabu ya Forest itakua imepata golikipa mzuri ambaye anaweza kuiweka imara milingoti ya klabu hiyo.Nottingham ForestTaarifa zinaeleza kua klabu ya Nottingham Forest bado inaangalia uwezekano wa kupata saini ya golikipa wa klabu ya Manchester United ambaye alikua klabuni hapo kwa mkopo msimu uliomalizika haswa katika wiki za mwisho za usajili.

Acha ujumbe