Winga matata wa klabu ya Everton Demarai Gray yuko kwenye hatua za mwisho za kujiunga na klabu ya Al Shabab inayoshiriki ligi kuu ya Saudia Arabia maarufu kama Saudian Pro League.
Klabu ya Everton imeshakubaliana na klabu ya Al Shabab juu ya mchezaji Demarai Gray huku jambo linalosubiriwa ni mchezaji huyo kukubali kujiunga na klabu hiyo ili dili hilo likamilike na kuelekea nchini Saudia.Mshambuliaji huyo anaweza akakubali ofa iliyowekwa mezani na matajiri hao kutoka nchini Saudia kwani vilabu hivyo hutoa ofa nono ambayo wachezaji wengi ulaya wameshindwa kukataa na kujiunga na vilabu vya Uarabuni.
Mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya Leicester City amekua kwenye kiwango kizuri ndani ya Everton, Lakini klabu ya Al Shabab imeonesha kuhitaji saini ya mchezaji Demarai Gray na vyanzo vinaeleza yuko mbioni kukubali ofa hiyo.