Manchester United Kuondolewa Sokoni

Wamiliki wa klabu ya Manchester United raia wa Marekani wanaojulikana kama Familia ya Glazer inaelezwa wana mpango wa kuitoa sokoni klabu hiyo.

Glazers waliiweka Manchester United sokoni mwishoni mwa mwaka jana na matajiri mablimbali walionesha nia ya kutaka kuinunua klabu hiyo, Lakini mchakato umechukua muda mrefu sana mpaka wamiliki hao wametaka kusitisha mchakato.manchester unitedFamilia ya Glazers wanaimiliki klabu hiyo tangu mwaka 2005 na wamefanakiwa kupata mafaniko ya kutosha na timu hiyo, Lakini siku za karibuni mashabiki wamekua hawawataki kutokana na muenendo mbovu wa timu hiyo.manchester unitedMashabiki wa klabu ya Man United wamekua wakiwashutumu wamiliki hao kua ndio chanzo cha klabu hiyo kufanya vibaya kutokana na uongozi wao mbovu ambao umepelekea sajili zisizo na tija klabuni hapo na timu hiyo kuanguka kwenye ubora wako.

Baada ya taarifa ya Glazers kutaka kuiondoa klabu hiyo sokoni na kuachana na mchakato wa kuiuza klabu hiyo, Swali limebaki kama wataweza kuhimili presha ya mashabiki wa Manchester United ambao wamekua wakiandamana kuwakataa wamiliki hao.

Acha ujumbe