Manchester United Yahamia kwa Reguilon

Klabu ya Manchester United imehamishia nguvu kwa beki wa klabu ya Tottenham Hotspurs Sergio Reguilon kwajili ya kumpata kwa mkopo wa msimu mzima.

Manchester United walikua wanamfukuzia Marc Cucurella wa klabu ya Chelsea, Lakini taarifa zinaeleza mpaka sasa nguvu wamehamishia kwa beki huyo wa kimataifa wa Hispania ambaye nae alikua kwenye orodha yao.manchester unitedSergio Reguilon ambaye ametoka kutolewa kwa mkopo msimu uliomalizika na msimu huu anahitajika na Man United kwa mkopo vilevile, Hii inatokana na mchezaji huyo kutopata nafasi ya moja kwa moja ndani ya klabu Tottenham.

Man United walikua wako mbioni kumsajili beki Marc Cucurella kutoka Chelsea lakini inaelezwa klabu ya Chelsea ndio wameweka ugumu dili hili kukamilika mpaka wakati huu  japo mazungumzo bado hayajavunjika mpaka sasa.manchester unitedManchester United wanahitaji mbadala wa beki wao wa kushoto Luke Shaw ambae amepata majeraha siku kadhaa nyuma, Hivo wamelazimika kumuhitaji beki Sergio Reguilon kutoka klabu ya Tottenham kwa mkopo wa msimu mzima.

Acha ujumbe