Klabu ya Manchester United inaelezwa kukataa kueleza habari juu ya mshambuliaji wao mpya raia wa kimataifa wa Denmark Rasmus Hojlund kama amefanya mazoezi na timu siku ya jana.
Manchester United wanaonekana hawataki ijulikane kama mchezaji huyo ameanza kufanya mazoezi na wenzake kuelekea mchezo wao wa jumapili dhidi ya klabu ya Arsenal na kutaka kushtukiza kumchezesha mchezaji huyo.Mshambuliaji huyo amejiunga na Man United akitokea klabu ya Atalanta alikua anaandamwa na majeraha madogo madogo hivo kumfanya kushindwa kucheza hata mchezo mmoja wa ligi kuu ya Uingereza mpaka sasa.
Kocha wa klabu ya Manchester United Erik Ten Hag alieleza siku kadhaa nyuma kua mshambuliaji Rasmus Hojlund anakaribia kurejea ndani ya klabu hiyo lakini bado hajaweka wazi atarejea siku gani.Mshambuliaji Rasmus Hojlund anasubiriwa kwa hamu kuonekana kiwanjani akiitumikia klabu hiyo katika michuano mbalimbali, Kutokana na imani kubwa ambayo mashabiki wa klabu hiyo wanayo juu ya mshambuliaji huyo.