Klabu ya Manchester United ni kama wanahaha kutafuta mbadala wa beki wake wa kushoto Luke Shaw baada ya kuhusishwa na beki Marc Cucurella wa Chelsea sasa wanahusishwa na Marcos Alonso kutoka Barcelona.

Manchester United wamejikuta kwenye hali ngumu baada ya mabeki wake wote wa kushoto kupata majeraha, Hivo wamelazimika kuingia sokoni kutafuta beki wa kushoto jambo ambalo halikua kwenye mipango yao mwanzoni mwa dirisha.manchester unitedTaarifa kutoka nchini Hispania zinaeleza kua Man United wameulizia huduma ya beki Marcos Alonso ambaye wanahitaji kumsajili lakini kwa gharama ya kawaida kwani ni usajili ambao umetokea kwa lazima na haukua kwenye mipango.

Mazungumzo yanaripotiwa kuendelea baina ya klabu ya Man United kwajili ya beki huyo raia wa kimataifa wa Hispania, Hivo kama mazungumzo yataenda mashetani wekundu watamchukua Marcos Alonso beki wa zamani wa klabu ya Chelsea.manchester unitedBeki Marcos Alonso amekua hapati nafasi ya kudumu ndani ya klabu ya Barcelona tangu asajiliwe dirisha kubwa lililopita na nafasi akipewa kinda Alejandro Balde,Hivo Marcos Alonso anaweza kuitumia fursa na kujiunga na Manchester United.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa