Klabu ya Manchester United imefanikiwa kupata alama tatu tena katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya klabu ya Nottingham Forest baada ya kutoka nyuma na kushinda kwa mabao matatu kwa moja.
Manchester United walianza kutanguliwa kwa mabao ya mapema ya Awoniyi na beki Willy Bolly, Lakini Man United walitoka nyuma na kupata matokeo ya ushindi kupitia magoli ya kiungo Christian Eriksen, Carlos Casemiro, na nahodha Bruno Fernandes.Man United walikua wametoka kupoteza mchezo wa mwisho wa ligi kuu ya Uingereza kabla ya leo dhidi ya klabu ya Tottenham ambapo walifungwa mabao mawili kwa bila, Lakini leo wamerudi na kuweza kupata matokeo ya ushindi nyumbani.
Vijana wa Erik Ten Hag licha ya kupata matokeo katika mchezo wa leo lakini bado wanaonekana hawajakaa kwenye kiwango kinachohitajika, Kwani kila eneo la uwanja linaonekana lina mapungufu kuanzia safu ya ulinzi, katikati na safu ya ushambuliaji pia.Manchester United wameendelea kulinda rekodi yao ya kutopoteza mchezo katika dimba la Old Trafford, Kwani klabu hiyo ilikua haijapoteza michezo 30 katika dimba hilo kwenye michuano yote lakini 19 kwenye ligi kuu ya Uingereza hivo baada ya matokeo ya leo wamefikisha michezo 31 kwenye michuano yote na 20 kwenye ligi kuu.