Arsenal Yadondosha Alama Dhidi ya Fulham

Klabu ya Arsenal imedondosha alama kwa mara ya kwanza msimu huu katika michezo ya ligi ya ligi kuu ya Uingereza baada ya kulazimishwa sare ya mabao mawili kwa mawili na klabu ya Fulham.

Katika mchezo ambao umepigwa katika dimba la Emirates ni Fulham ambao walitangulia kupata bao kabla ya Arsenal kusawazisha na kuongeza bao la pili kabla ya Fulham kurudi na kusawazisha ubao na kufanya matokeo kua sare.arsenalWashika mitutu wa London walifanikiwa kushinda michezo yao miwili ya awali ya ligi kuu ya Uingereza, Lakini leo mchezo kati na Fulham ulikua mgumu na kufanya kuambulia alama moja kati ya alama tatu walizokua wanagombania.

Vijana wa Marco Silva licha ya mchezaji wao Calvin Bassey kuoneshwa kadi dakika ya 83 ya mchezo wakiwa nyuma kwa mabao mawili, Lakini hawakuacha kuonesha ubora mpaka dakika ya 87 walipofanikiwa kusawazisha kupitia kiungo Palhinha.arsenalKlabu ya Arsenal kupitia kocha Mikel Arteta waliamini walistahili kupata matokeo katika mchezo wa leo lakini bahati haikua upande wao, Wakati huohuo mchezo unaofuata wa klabu hiyo ni dhidi ya klabu ya Manchester United.

Acha ujumbe