Dean Henderson Aelekea Crystal Palace

Golikipa wa klabu ya Manchester United Dean Henderson raia wa kimataifa wa Uingereza amekamilisha usajili wake wa kujiunga na klabu ya Crystal Palace baada ya kufikia makubaliano.

Golikipa Dean Henderson alikkua anahusishwa kurejea klabu ya Nottingham Forest ambapo alikua anaitumikia klabu hiyo kwa mkopo msimu uliomalizika, lakini Crystal Palace wameonekana kushinda mbio hizo na kumchukua golikipa huyo.dean hendersonBaada ya Manchester United kufikia makubaliano na Crystal Palace ya kumuuza kipa wao huyo chaguo la pili kwasasa wanakaribia kukamilisha usajili wa golikipa Altay Bayindir kutoka klabu ya Fenerbahce kama mbadala wa golikipa huyo wa kimataifa wa Uingereza.

Golikipa huyo ambaye amewahi kuvitumikia vilabu vya Nottingham Forest na Sheffield United kwa mkopo sasa anaondoka ndani ya klabu ya Manchester United baada ya miaka 12 ambayo amekua na klabu hiyo toka timu ya vijana.dean hendersonSababu kubwa ya golikipa Dean Henderson kutaka kuondoka ndani ya Man United ni kutaka nafasi ya kucheza zaidi, Kwani golikipa huyo hakuwahi kupata nafasi ya kua golikipa namba moja ndani ya klabu hiyo fursa ambayo alikua anaiihitaji ili aweze kubaki kwenye timu hiyo.

Acha ujumbe