Winga wa klabu ya Liverpool Mohamed Salah inadaiwa anahitaji kuondoka ndani ya klabu hiyo baada ya kuhitajika na mabingwa wa soka nchini Saudia Arabia klabu ya Al-Ittihad.
Mohamed Salah inaelezwa ameridhishwa na ofa iliyowekwa mezani na mabingwa hao wa soka nchini Saudua na yeye mwenye akitaka kutimka katika viunga vya Anfield.
Klabu ya Al-Ittihad inaonesha imedhamiria kutetea taji lake ambalo imetwaa msimu uliomalizika kutokana na sajili ambazo wamekua wakizifanya hivi karibuni.
Baada ya Al-Ittihad kuonesha nia ya kumtaka staa huyo wa kimataifa wa Misri na mshambuliaji huyo kuvutiwa na ofa ya klabu hiyo, Kibao kimegeuka kwani taarifa zinaeleza Mohamed Salah sasa ndio analazimisha kuondoka katika klabu hiyo.
Kocha wa Liverpool alihojiwa siku kadhaa nyuma baada ya taarifa hizi kutoka na kocha huyo alionesha bado wanamuhutaji mchezaji huyo zaidi kwenye timu hiyo na hawawezi kumuuza, lakini taarifa za ndani zinaeleza Liverpool wanakaribia kukubali ofa ya Al-Ittihad baada ya mchezaji mwenye kukubali kutimka.

