Mchezaji nyota wa klabu ya Liverpool Mohamed Salah amewaondoa wasiwasi mashabiki wa timu kuhusu tetesi za kutaka kuondoka kwenye klabu hiyo na kuwahakikishia kuwa bado ataendelea kuwepo kwa msimu ujao.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Misri mpaka sasa bado hajasaini mkataba mpya na miamba hiyo ya Anfield ambapo mkataba wake wa sasa unakwenda kuisha mwaka 2023 june.

Mohamed Salah
Mohamed Salah

Liverpool wanaweza kumpoteza Mohamed Salah bure kwenye dirisha la usajiri la majira ya kiangazi mwaka 2023, ikiwa hata saini mkataba mpya mpaka mwishoni mwa msimu ujao. Lakini Salah amethibitisha kuwa ataendelea kuwepo kwenye klabu hiyo kwa miezi 12 minngine.

Mohamed Salah akizungumza kabla ya mchezo wa fainali ya ligii ya mabingwa jumamosi dhidi ya Real Madrid, alisema; “Ninabaki kwa msimu ujao kwa hakika.

“Sijajikita kwenye mkataba kwa kwenye kipindi hiki. Ni kuhusu timu, kwa kweli ni wiki muhimu kwetu, nataka kushinda kombe la ulaya tena.

“Nataka kumuona Hendo (Jordan Henderson) akiwa na kombe mikononi mwake tena na nina matumaini atanikabidhi mimi.”

Mohamed Salah ameshinda kombe la ligi kuu ya Uingereza, kombe la ulaya, FA Cup, kombe la ligi, Super Cup na kombe la dunia la vilabu mafanikio yote haya ameyapata ndani ya miaka mitano.

Liverpool walilipa kiasi cha £36.5 million kama ada ya uhamisho ili kuwaza kumrudisha nyota huyo wa zamani wa Chelsea .

Salah amefanikiwa kuifungia klabu ya Liverpool magoli 156 kwenye michezo 253 kwa kipindi chote alichokuwepo kwenye klabu hiyo mpaka sasa.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa