Wakati suala la Mo Salah kusalia/kuondoka Liverpool likiwa limebaki kwenye mlinganyo, wakongwe waliowahi kucheza kwenye klabu hiyo watoa neno.

Salah amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake wa sasa na, mazungumzo ya mkataba mpya hayaonekani kutoa mwangaza kwa pande zote zinazohusiana na sakata hili. Kulikoni?

Miongoni mwa wakongwe waliopita kwenye klabu ya Liverpool ni Jamie Redknapp. Yeye anadhani kati ya wachezaji wote wa Liverpool, anayestahili kulipwa mshahara mrefu ni Virgil Van Djik pekee.

Wakongwe, Wakongwe Liverpool Watoaneno Kwa Salah, Meridianbet
Jamie Redknapp

Redknapp anaamini, ni rahisi sana kumpata Salah mwingine kuliko kumpata Van Djik mwingine kwenye soka la sasa. Japokuwa kunakasumba ya kuwathamini zaidi washambuliaji, walinzi ni watu wa muhimu zaidi na adimu sokoni. Kwa misingi hii, haoni sababu ya Salah kuwaumiza vichwa viongozi wa Liverpool hasa kwenye maslahi.

Maneno ya Redknapp yanaongezewa nguvu na mkongwe mwingine miongoni mwa wakongwe wa Liverpool, Jamie Carragher ambaye yeye anamuasa Salah, asitegemee kwamba maisha ni marahisi nje ya Liverpool. Carragher anamueleza Salah kuwa, Liverpool ndio imempa ‘ustar’ alionao. Ajifunze kwa baadhi ya wachezaji ambao walidhani ustar wao ungewapa faida nje ya Liverpool.

Wakongwe, Wakongwe Liverpool Watoaneno Kwa Salah, Meridianbet
Jamie Carragher

Philippe Coutinho, Gini Wijnaldum na Emre Can, ni baadhi ya wachezaji ambao walikuwa wakawaida sana walipojiunga na Liverpool lakini, chini ya Jurgen Klopp, walipata ustar na baadae kuamua kuondoka kwa sababu za kimaslahi. Hawa watatu, wote hawapo tena na ustar wao na wala hawana mafanikio waliyoyapata walipokua Anfield.

Mo Salah, asiyesikia la mkuu, huvunjika guu. Waswahili husema, “akili kumkichwa”


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa