Ronaldo Mchezaji Bora wa Mwezi Saudia

Staa wa klabu ya AL Nassr inayoshiriki ligi kuu nchini Saudia Arabia maarufu kama Saudian Pro League Cristiano Ronaldo ametangazwa kua mchezaji bora wa mwezi wa nane wa ligi hiyo.

Ronaldo anafanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi nchini Saudia kutokana na kiwango alichokionesha ndani ya mwezi Agosti kwenye ligi kuu nchini Saudia Arabia ambapo ameweza kuhusika katika mabao saba ndani ya mwezi huo.ronaldoKlabu ya Al Nassr ilianza vibaya katika ligi baada ya kuanza na vichapo katika michezo miwili ya awali, Lakini ilifanikiwa kuamka na kupata matokeo ya ushindi katika michezo yake iliyofata tena kwa idadi kubwa ya mabao.

Staa huyo zamani wa vilabu vya Man United, Real Madrid, na Juventus amefanikiwa kufunga mabao matano katika mwezi huku akifanikiwa kuoiga pasi mbili zilizozaa mabao na zote zilielekea kwa mchezaji mwenzake Sadio Mane na kumfanya kuhusika kwenye mabao saba.ronaldoMshambuliaji Cristiano Ronaldo tangu ametua nchini Saudia Arabia amekua mchezaji muhimu sana ndani ya kikosi cha Al Nassr na kufanikiwa kuisaidia klabu hiyo kutwaa taji la michuano ya Arabs mwezi mmoja uliomalizika.

 

Acha ujumbe