Reguilon Kukipiga Man United

Beki wa kushoto wa klabu ya Tottenham Hotspurs raia wa kimataifa wa Hispania Sergio Reguilon anakaribia kukamilisha dili lake la kujiunga na klabu ya Manchester United.

Beki Sergio Reguilon alikua kwenye orodha ya mabeki ambao Manchester United wanapanga kuwachukua kama mibadala ya beki Luke Shaw akiwemo na beki Marc Cucurella, na Marcos Alonso lakini beki huyo wa Tottenham ndio amefanikiwa kua kinara na kujiunga na United.reguilonKlabu ya Manchester United ilikua karibu kwenye mazungumzo na klabu ya Chelsea mpaka usiku wa jana lakini taarifa zinaeleza kua Chelsea walikua wanatia ugumu dili hilo kukamilika na ndio sababu Man United wakahamia kwa beki huyo wa Spurs.

Beki huyo wa klabu ya Tottenham inaelezwa anajiandaa kuelekea jijini Manchester wakati huu kwenda kuchukua vipimo vya afya ambapo tayari ameshaiomba ruhusa kwa klabu yake ya Tottenham.manchester unitedDili la Sergio Reguilon kujiunga na Man United liko katika hatua za mwisho kabisa kwani tayari kumeshakua na makubaliano baina ya pande zote mbili,Yaani upande wa vilabu na upande wa mchezaji ambae ameshakubaliana na Man United.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.