Kocha wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola ameingia kwenye kinyang’anyiro cha kuwania tuzo ya kocha bora wa mwaka akiwa na makocha wengine wanne.
Pep Guardiola anaungana na makocha wengine kama Simeone Inzaghi wa Inter Milan, Luciano Spalletti aliyekua kocha wa Napoli sasa timu ya taifa ya Italia, Ange Postecoglou Tottenham Hotspurs, na Xavi Hernandez wa klabu ya Barcelona.Kocha Pep Guardiola alikua na mafanikio makubwa msimu uliomazika akifanikiwa kuiongoza timu hiyo kutwaa mataji matatu ikiwemo ligi kuu ya Uingereza, ligi ya mabingwa barani ulaya, na kombe la Fa na mpaka sasa ndio kocha anaepewa nafasi zaidi ya kushinda.
Makocha wengine walioingia kwenye kinyang’anyiro hicho ni Simeone Inzaghi ambaye alikua na msimu mzuri ndani ya Inter Milan akiiongoza klabu hiyo kufika fainali ya ligi ya mabingwa ulaya na kocha Ange ambaye alikua Celtic msimu uliopita akifanikiwa kuiongoza klabu hiyo kutwaa ubingwa.Kocha Xavi Hernandez yeye alifanikiwa kuiongoza klabu ya Barcelona kutwaa taji la ligi kuu ya Hispania na kombe la Spanish Super Cup, Huku kocha Luciano Spaletti ambaye anaiongoza timu ya taifa ya Italia alifanikiwa kuiongoza klabu ya Napoli kutwaa taji la ligi kuu ya Italia.