Guardiola: Bado Tunamuhitaji Walker

Kocha wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola amesema bado kama klabu wanamuhitaji beki wa kulia wa klabu hiyo Kylie Walker aendelee kusalia ndani ya klabu hiyo.

Kylie Walker anahusishwa kutimka ndani ya klabu hiyo huku akihusishwa kutimkia klabu ya Fc Bayern Munich ya Ujerumani ambayo imeonesha nia ya kumsajili, Lakini Guardiola anaamini bado wanaweza kumbakiza mchezaji huyo.GuardiolaKylie Walker amekua mchezaji muhimu tangu ametua klabuni hapo akitokea Tottenham Hotspurs, Huku taarifa zikieleza beki huyo anataka kutafuta changamoto klabu nyingine na Bayern wako mstari wa mbele kumuhitaji mchezaji huyo.

Guardiola pamoja na klabu ya Manchester City wanatamani kumbakiza Walker ndani ya viunga vya Etihad, Kinachosubiriwa ni kuangalia nani atashinda mtanange wa kumshawishi mchezaji huyo kati ya Man City na Bayern Munich.GuardiolaKylie Walker kama atafanikiwa kutimka ndani ya klabu Manchester City basi klabu hiyo italazimika kuingia sokoni kutafuta mbadala wa mchezaji huyo na hivi karibuni wamefikia makubaliano ya kumuongezea mkataba beki wake Nathan Ake.

Acha ujumbe