Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United raia wa kimataifa wa Ufaransa Anthony Martial amerejea kwenye mazoezi ya klabu hiyo baada ya kutoka majeruhi.

Anthony Martial amerejea mazoezini ndani ya klabu hiyo ambapo alikaa nje ya uwanja kidogo na kukosa michezo mitatu ambayo klabu ya Man United imecheza kujiandaa na msimu mpya katika nchi za Norway, Scotland, Marekani.MartialKocha wa Manchester United Erik Ten Hag ameuongelea urejeo wa mshambuliaji huyo akisema kua anahitaji ubora kwenye kikosi chake, Huku mshambuliaji huyo akiwa ni bora na ataisaidia sana timu hiyo kama atakua fiti bila majeraha.

Staa huyo wa kimataifa wa Ufaransa amekua akiandamwa na majeraha mara kwa mara kwenye klabu hiyo, Hivo kocha huyo anaona kama mchezaji huyo atakua uwanjani bila majeraha basi ataweza kuisaidia sana klabu hiyo.MartialAnthony Martial amekua akiuliziwa na vilabu kadhaa kutoka nchi za kiarabu wakitaka huduma yake, Lakini kutokana na maelezo ya kocha wa klabu hiyo Erik Ten Hag ameonesha bado ana imani kubwa na mchezaji huyo kuelekea msimu ujao.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa