Huku tetesi za usajili zikiendelea kupamba moto taarifa zinasema kuwa mchezaji wa Ajax Edson Alvarez anakaribia kujiunga na Chelsea, huku mchezaji huyo akicheza katika nafasi ya kiungo.

Chelsea walifanya mbinu ya kumsajili kiungo huyo wa kati mwishoni mwa dirisha la usajili la majira ya kiangazi, lakini ofa yao ilikataliwa na Ajax na sasa mchezaji huyo wa Kimataifa wa Mexico pia anaivutia United ambayo inaweza kuanzisha vita ya kumsajili.
Majira ya joto yaliyopita, klabu ya Ajax iliona uhamisho mkubwa wa wachezaji uliofanyika kutoka klabuni kwao ikiwa ni pamoja na mauzo ya Ryan Gravenberch, Lisandro Martinez na Antony hivyo ikawa ngumu kwao kumuachia kiungo huyo.

Kuelekea mwisho wa dirisha la usajili, Chelsea ilitoa ofa kwa ajili ya huduma ya Alvarez inayodaiwa kuwa na thamani ya pauni milioni 43.5. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 alitamani sana dili hilo kukamilika na akataka kulazimisha uhamisho wake kwenda Stamford Bridge kwa kukataa kuhudhuria mazoezi.
Lakini baada ya uhamisho huo kuonekana kushindikana, hivi majuzi Alvarez alitoa ya moyoni na kusema kuwa amesikitishwa na uhamisho wake kutokamilika na anatarajia klabu kubwa yoyote kwenda kumnunua.

Pia aliongeza kwa kusema kuwa; “Hatukutarajia Chelsea kuweka ofa nyingine mwishoni mwa Agosti. Ilikuwa hali ngumu na Ajax haikuweza kufanya lolote, na kwa upande mwingine inanipa motisha kubwa na kwamba vilabu vya ukubwa huo hufuatilia mechi zangu, na vitendo vyangu”.

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.
BONYEZA HAPA

