Klabu ya Liverpool ambayo ipo chini ya kocha mkuu Jurgen Klopp wanapanga kumnunua kiungo wa RB Leipzig Konrad Laimer kwaajili ya kuimarisha kikosi chao katika eneo la kiungo.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 alikuwa pia akitakiwa na wababe wa Ujerumani Bayern Munich katika majira ya joto lakini hatua hiyo ilishindikana wakati dirisha lilipofikia tamati.
Sky Germany wanaripoti kuwa Majogoo wa Anfield wamekuwa wakimfuatilia kwa karibu mchezaji huyo wa Kimataifa wa Austria huku kandarasi yake ikitarajiwa kumalizika mnamo 2023.
Nyota huyo amekuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Leipzig kilichomaliza katika nafasi ya nne kwenye Bundesliga msimu uliopita huku kiungo huyo akiwa na uwezo mkubwa sana kiasi ambacho kinawavutia vilabu vikubwa akiwemo Liverpool.

Laimer alifunga mara nne na kusaidia kama wengi katika kampeni ya 2021-22 licha ya kucheza nafasi ya kushikilia.
Mchezaji huyo wa Kimataifa mwenye mechi 24 ameichezea Leipzig mara 167 na hakuna uwezekano wa kusaini mkataba mpya huku akitafuta changamoto mpya katika maisha yake ya soka.

Na kama Fabinho, Jordan Henderson na Thiago Alcantara wote wanaelekea kustaafu, Laimer anaweza kuwa mbadala mzuri katika safu ya kiungo.

