Usajili: Hatma ya Lingard na Pereira ni Ipi?

Wakati huu ambapo dirisha la usajili likiendelea kutumika vyema kwa vilabu mbalimbali duniani. Tuangazie kidogo kikosi cha Man United chini ya Ole Gunnar Solskjaer.

Tangu kuanza kwa harakati za uhamisho wa wachezaji, Man United wamekuwa wakihusishwa na wachezaji mbalimbali. Sancho akiwa ameteka taarifa za kujiunga na timu hiyo, jambo ambalo mpaka sasa halieleweki.

Kunani Man United kwenye dirisha hili la Usajili?

Taarifa zinasema Donny Van De Beek ameshamaliza vipimo vya afya na huenda Man United wakatoa taarifa rasmi ya kumsajili kiungo huyu kutoka Ajax kwa ada ya pauni milioni 40.

Kutua kwa Van De Beek kutakuwa ni panga la moto kwa Lingard na Pereira kwani wanaendelea kuwa wachezaji wasio na namba kwenye kikosi cha Ole Gunnar Solskjaer.

Ujio wa Mholanzi huyo utaongeza nguvu kwenye safu ya kiungo ambapo tayari kuna wachezaji kama Juan Mata, Nemanja Matic, Scot McTominay, Fred, Bruno Fernandes na Paul Pogba. Kwa uwezo wa wachezaji hawa, ni dhahiri Lingard na Pereira hawana namba.

Kwa msimu uliopita, Lingard na Pereira wamecheza mechi chache sana kutokana na kutopata namba kwenye kikosi hicho, mara nyingi wamekuwa wakisugua benchi katika mechi za michuano yote. Huenda dirisha hili la usajili likawa ndio sehemu yao ya kuponea na sasa wanauwezekano mkubwa wa kuwekwa sokoni na Man United.

Ama kweli hakuna mwanzo usiokuwa na mwisho. Lingard alijunga na Man United akiwa na miaka 7 wakati Pereira alijiunga akiwa na miaka 15, sasa hivi wote wapo katika hali ya sintofahamu katika kikosi cha Ole Gunnar Solskjaer.


SHINDA NA HI LO

Sasa hii ni rahisi zaidi kupata USHINDI! Unatabiri karata ipi ipo chini au juu, kisha unakusanya mkwanja wako.

Cheza sasa

47 Komentara

    kwa inavyooneka man hawana mpango tena na hao wachezaji

    Jibu

    Man u bado kabic kwenye usajiri wanatakiwa wajipange sana ili kukamilisha kikosi chao

    Jibu

    Asanteni kwa taarifa

    Jibu

    Dah kwa hili man mtulie kidogo

    Jibu

    wawaache tu waendelee kusalia united

    Jibu

    Man u wanatakiwa wafanye kazi ya ziada ili kukamilisha kikosi chao zaidi

    Jibu

    Lingard na pereira watafute sehemu ya kwenda kwa man u awana chao

    Jibu

    Asanteni kwa taarifa meridianbet.

    Jibu

    Wabaki Man U

    Jibu

    Lingard ndo kwisa habari yake Uingereza sasa atamfuata Oscar China hukoo

    Jibu

    Kwangu Jesse Lingarda aondoke lakini Perreira apewe muda zaidi kwasabu msimu uliopita hakucheza vya kutosha#meridianbettz

    Jibu

    Asante kwa taarifa

    Jibu

    Lingard mda wake sasa kuondoka man u

    Jibu

    United kwenye swala la usajili wanaleta siasa

    Jibu

    Kwa msimu uliopita, Lingard na Pereira wamecheza mechi chache sana kutokana na kutopata namba kwenye kikosi hicho, mara nyingi wamekuwa wakisugua benchi katika mechi za michuano yote. Huenda dirisha hili la usajili likawa ndio sehemu yao ya kuponea na sasa wanauwezekano mkubwa wa kuwekwa sokoni na Man United.

    Jibu

    Man U mnakwama wapi tena mbona mnayumba kwauyo dogo

    Jibu

    Lingard na perreira sasa ya tosha watafute timu ya kucheza tu

    Jibu

    Habarii nimeielewa

    Jibu

    Wabaki man tu

    Jibu

    Asnt kwa taarif

    Jibu

    Ni vyema wakatfute timu ya kucheza

    Jibu

    wabaki man tu

    Jibu

    mashabiki wa man united hatuelewi usajili wa sancho

    Jibu

    Duuh noma sana.

    Jibu

    Aisee hii ni hatari

    Jibu

    Kama hawafai watoke tu

    Jibu

    Lingad alikuja moto Sana Ila sasa anaonekana hafai.

    Jibu

    Watafute machaka mengine

    Jibu

    Cjaelewa vzur hii

    Jibu

    Man u hawana jipya bhana

    Jibu

    Man u inaitaji watu wazoef km hawa so kina lingard

    Jibu

    Ni lingard ni mchezaj makin sana ila majeruh yanamkosti

    Jibu

    Habari njema

    Jibu

    Mambo ya soka hayoo!!!

    Jibu

    Habari njema

    Jibu

    Lingard kwa man u Hana namba.

    Jibu

    Mashabiki tunashukuru kwa taarifa
    @meridianbettz

    Jibu

    Ahsante kwa makala na meridian.

    Jibu

    Habari nzuri

    Jibu

    kikosi hicho, mara nyingi wamekuwa wakisugua benchi katika mechi za michuano yote. Huenda dirisha hili la usajili likawa ndio sehemu yao ya kuponea na sasa wanauwezekano mkubwa wa kuwekwa sokoni na Man United.

    Jibu

    Habari njema

    Jibu

    Nihabari njema

    Jibu

    Maamuzi yao wenyewe

    Jibu

    Asante kwa nakala

    Jibu

    Habari nzuri sana

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.