US Open: Osaka na Djokovic Waendelea Kung'ara

Mashindano ya US Open yameanza kwa kasi. Wakati huu ambapo nyota kadhaa wa mchezo wa tenisi wakikosekana, wapinzani wao wanautumia mwanya huu kuonesha uwezo wao kunako mchezo wa tenisi.

Naomi Osaka na Novak Djokovic ni kati ya wachezaji nyota wa tenisi wanaoshiriki michuano hiyo kwa mwaka huu. Rafael Nadal, Rodger Federer, Andreescu ni kati ya nyota wanaokosekana msimu huu.

US Open imeanza kwa kasi ya aina yake.

Naomi Osaka ameanza kwa kumburuza mpinzani wake Misaki Doni kwa kupata ushindi wa pointi 6-2 5-7 6-2

Naomi Osaka

Wakati ambapo Osaka akisogea kwenye hatua inayofuata, Coco Gauff alijikuta akitolewa na Anastasija Sevastova kwa seti 6-3 5-7 6-4.

“Ulikuwa ni mchezo mgumu. Nilijua kuna uwezekano mchezo ungekuwa mrefu, nitaangalia itakavyokuwa kesho.” amesema Naomi Osaka.

Novak Djokovic alikuwa na wakati mzuri baada ya kumfunga Damir Dzumhur kwa seti 6-1 6-4 6-1

Kwa matokeo haya, Djokovic atakutana uso kwa uso na Kyle Edmund katika mzunguko wa pili. Hii itakuwa ni mara ya 7 kwa wachezaji hawa kukutana huku Edmund akiwa ameshinda mara 1 pekee mwaka 2018.

Novak Djokovic

“Anaweza kusevu vizuri na pia ana mkono mwepesi, hizo ndio silaha zake kubwa. Nimekuwa na michezo mizuri dhidi yake kwa miaka ya nyuma kwenye Wimbledon, mchezo mgumu ulikuwa wa seti 4 miaka kadhaa iliyopita.

“Hasumbuliwi na msukumo wa kucheza michezo mikubwa. Hii ni hali ya tofauti lakini haimsumbui kwa sababu anapenda changamoto.

“Amekuwa na matokeo ya kupanda na kushuka lakini ninadhani anamchezo mzuri na ananafasi ya kuwa kati ya wachezaji 20 bora bila shaka, ninategemea atakua huko siku sio nyingi..

“Utakuwa ni mchezo mgumu. Najua hajajianda kuja kupoteza mchezo. Na mimi pia ninajiandaa ili nipate matokeo mazuri.” amesema Novak Djokovic.

Wapinzani wa kubwa kwa Djokovic msimu huu ni Alexander Zverev na Stephanos Tsitsipas baada ya wachezaji hao kushinda michezo yao ya kwanza kunako Mashindano ya US Open.


SHINDA NA HI LO

Sasa hii ni rahisi zaidi kupata USHINDI! Unatabiri karata ipi ipo chini au juu, kisha unakusanya mkwanja wako.

Cheza sasa

20 Komentara

    pongezi nyingi sana kwao waendelee kufanya juhudi ili wafike mpaka fainal

    Jibu

    Ulikuwa mchezo mgumu sana kwa naomi usaka ingawa alijitahidi

    Jibu

    Hongera zao

    Jibu

    Tenis msimu huu kuna mabadiliko mkubwa tuzoea kuwaona wakina Serena amakweli kutesa kwa zamu

    Jibu

    pambano lilikua la aina yake

    Jibu

    Pongezi sana kwao

    Jibu

    Mungu awajalie

    Jibu

    Hongera zao

    Jibu

    Wametisha sanaa

    Jibu

    Wametisha sana

    Jibu

    Hongera yao jmn

    Jibu

    ndo wakati wao huu kuonyesha mashabiki vipaji vyao tuone

    Jibu

    Naomi Osaka namkubali sana.

    Jibu

    Vzr sana

    Jibu

    Wako vizuri

    Jibu

    Hongera zao.

    Jibu

    Wako vizuri

    Jibu

    Wametisha kwa rekodi nzuri

    Jibu

    Rekodi nzuri Sana

    Jibu

    Hongera zao

    Jibu

Acha ujumbe