Ligi ya Uingereza ni kati ya ligi zinazofuatiliwa sana na watu ulimwenguni kote. Kitu hicho kinaifanya ligi hiyo iweze kuwa maarufu zaidi siku zote. Lakini pia inaheshimika kwa kuwa na wachezaji wenye majina makubwa kama Eden Hazard, Kane, Pogba na wengineo; lakini nyuma ya wachezaji hao kuna watu wanaowafanya wao kuonekana bora kama ilivyo hivyo leo.
Hii inafananishwa na uwepo wa Busquets pale Barcelona ambapo kunamfanya Messi aonekane bora sana kutokana na kulishwa mipira mingi na kuwa na muunganiko mzuri kati ya safu ya ushambuliaji na ile ya kiungo. Jambo hilo ndilo hufanya soka kuwa na mvuto wa pekee siku zote. Lakini pia, Uingereza kuna majina ambayo yanapewa heshima ndogo lakini wana mchango mkubwa sana ndani ya vikosi vyao:
Victor Lindelof
Kazi yake ni kubwa sana ndani ya Manchester United. Ameweza kuimarisha safu ya ulinzi ya klabu hiyo tangu alipojiunga kutokea Benfica. Kwa hakika anapaswa kupewa heshima yake kwa hilo kwani ameweza kuifanya safu ya ulinzi hiyo kujengeka upya baada ya kipindi kirefu cha kuhangaika kupata mbadala wa safu hiyo muhimu.
Aymeric Laporte
Uwepo wa watu kama David Silva, Arguero, Kevin de Bruyne unamfanya asipate heshima yake kwa sasa. Lakini amekuwa muhimili mkubwa katika eneo la ulinzi kwa kusaidia kutoruhusu kufungwa magoli mengi ndani ya kikosi chao hicho. Lakini kati ya wachezaji wenye mchango mkubwa kikosini hapo hawezi kutajwa kutokana na imani ya mashabiki wa soka.
Cesar Azpilicueta
Ana misimu saba hadi sasa ndani ya Chelsea, klabu ambayo ameisaidia katika namna nyingi hadi leo klabu hiyo haijawahi kufikiria kuhusu safu ya ulinzi, hilo ni kutokana na uwepo wake na kutoa msaada mkubwa anaoendelea kuutoa kikosini hapo. Ameweza kucheza klabuni hapo na kuaminiwa na makocha wote waliopita hapo. Lakini upande wa pili hawezi kuhusishwa sana kama ni bora kutokana na matunda hayo.
Georginio Wijnaldum
Alitua LFC kutokea Newcastle mwaka 2016. Huku akiwa na mwenendo mzuri sana katika ligi hiyo. Kazi yake inaonekana na hakuna anayeweza kubisha uwezo wa mchezaji huyo katika kulitawala eneo la kiungo. Japo hapewi heshima anayostahili kwenye hilo.
Jan Vertonghen
Uimara wa safu ya ulinzi wa Tottenham ni kutokana na uwepo wa wachezaji wa aina yake anajua majukumu yake na yanaisaidia Spurs kupata matokeo mazuri mara nyingi.


Povel
Gud news
isha
Makala safi
Njiku
Safiii hii