Mkongwe katika majukumu ya umeneja wa klabu za soka, Jose Mourinho ambaye alitimuliwa na Manchester united mwishoni mwa mwaka uliopita anasema anataka kurejea kwenye umeneja msimu ujao.
Meneja huyu amekiri wazi uhitaji wake wa kuchukua kibarua kipya na kutaja kuwa angependelea zaidi kuwa meneja wa klabu za Ligue 1. Akiwa kama mchambuzi wa fainali ya Carabao Cup kwenye kituo cha DAZN Spain, mreno huyu anasema anatarajia kurejea kwenye majukumu ya umeneja msimu ujao wa joto.
Wiki iliyopita Mourinho alinukuliwa akisema kuwa alikuwa anavutiwa kuingia League 1 baada ya ukweli kuwa amefanikiwa kuzunguka katika ligi kadhaa kama kiongozi, hivyo nafasi ya kuingia Ligue 1 kwake ni nafasi ya msingi anayoitamani.

“Najiona nikiwa nafundisha Ufaransa (Ligue 1) siku moja, mimi ni mtu niliyefanya kazi katika nchi tofauti 4 na ninayependa utamaduni mwingine. Napenda sana kujifunza na kufanya kazi katika nchi nyingine itakuwa ni jambo jema sana.” -Mourinho


Zeiyana
Mourinh ni kocha mwenye ndoto zake