Balotelli Mbioni Kuitwa Kikosini Taifa!

Mario Balotelli yupo mbioni kuitwa kuitumikia timu yake ya Taifa! Meneja wa timu ya taifa ya Italia Roberto Mancini amethibitisha kuwa anamfuatilia kwa ukaribu zaidi nyota huyu kujua kama anaweza kumuita kupambania taifa lake kufuzu michuano Euro 2020.

Nyota huyu hajaichezea timu ya taifa ya Italia toka mwezi Septemba mwaka jana. Hata hivyo nyota huyu ameweza kuchapa magoli 3 kwa gemu 4 alizowachezea Olympique Marseille. Mancini anasema nyota huyu ameanza vyema katika kumshawishi kumuita kikosini.

Meneja huyu pia amegusia kuhusu muenendo wa matokeo wa timu ya Italia akisisitiza kuwa timu hiyo inahitaji mda ili kuweza kurejea kunye ushindi wa uhakika. Mda na wachezaji sahihi ni kitu muhimu meneja huyu anaamini wako kwenye msatari kuelekea mafanikio.

“Malengo yetu ni kukikusanya pamoja kikosi bora kitakachoweza kufanya vizuri kwenye Euro. Hapana sahaka, Italia inahitaji kushiriki wakati wote tukiwa na nia ya kushinda.” –Mancini akizungumzia kikosi.

“Mario ameanza vyema kwa kufunga magoli 3 kwenye mechi 4 za Marseille. Narudia, tunamfuatilia kwa ukaribu kama tunavyowafuatilia wengine.” -Mancini akimzungumzia Balotelli

Acha ujumbe