Tuko Gado kwa Lolote -Lukaku

Klabu ya Manchester United wanaendelea kujiweka kuwa bora zaidi. wakiwa wanafanya vyema katika matokeo yao ya hivi karibuni toka wawe chini ya Ole Gunnar huku matokeo pekee mabaya zaidi kuyapata yakiwa ni kwenye gemu ya Ligi ya Mabingwa wakitandikwa bao 2 na PSG. Lukaku bado anasisitiza klabu hiyo iko Gado kwa lolote.

Licha ya matumaini ya Ole Gunnar kuwa Lingard na Martial wote wangeingia dimbani dhidi ya Liverpool, haikuwa hivyo kwa sababu martial hakuweza kuingia dimbani wakati Lingard akiingia kutokea benchi. Jitihada za ushindi hazikuzaa matunda kwa wababe wanaoongoza ligi na kulazimika kugawana pointi moja moja.

Matokeo haya yamewaacha Manchester United wakirejea mtaa wa 5 na Arsenal wakitoboa kurudi mtaa wa 4 kwenye msimamo wa Ligi wakati Manchester City naye akirejea nafasi ya pili akitofautiana pointi 1 na vinara wa ligi Liverpool.

Lukaku anasema kuwa ni anaona safu ya wakufunzi wao inafanya kazi nzuri na kuwaandaa kutokuwa waoga katika hali yeyote hata wanapokuwa na majeruhi. Klabu hii inatarajia makubwa, Ole Gunnar anasema licha ya watu kutegemea ushindi zaidi kwa klabu hiyo, wao wanaamini wanakuwa bora kwenye safu ya ulinzi na watafanya makubwa.

3 Komentara

    Thnks meridian bet kwa updates za michezo

    Jibu

    Ni kweli kabisa coz lukaku yuko vizuri sana.

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.