Gemu ya fainali ya Carabao Cup imewaacha chelsea wakipoteza matumaini ya kunasa taji msimu huu huku kukiwa na ushindani mkubwa kwa gemu zote. Wakati gemu ikiwa ngumu na wababe wakichuana vlivyo jana kulikuwa na sintofahamu baada ya golia Kepa Arrizabalaga kudaiwa kugomea sabu ili acheze vipindi vyote na dakika za nyongeza.
Kepa alilazimika kupata matibabu mara mbili kwenye dakika za nyongeza ili aweze kumalizia sehemu ya mtanange iliyobaki. Lakini alipotakiwa kutoka hakutaka huku madaktari wake wakidai kuwa alikuwa na shida ndogo wakati yeye akisema kuwa alikuwa hana shida yeyote ya kumkwamisha zaidi.
Licha ya Jitihada za chelsea kuhakikisha wana kinyaka kikombe hiki kama taji la kwanza la msimu huu, hawakuwa na bahati baada ya dakika zote 120 kuwaacha miamba yote miwili ikiwa haijaona lango la mwenzie. Mikwaju ya penati iliyoamua mshindi ilimuacha Kepa akiruhusu mkwaju mmoja zaidi uliokamilisha bao 4-3 na kuwapa ushindi Manchester City.
Manchester City sasa wanatafuta kujikusanyia vikombe 4 kwa msimu huu kwa michuano yote wanayoshiriki na safari imeanza wakiwa wanakabiliwa na ushindani mkali kwenye Ligi Kuu ya Uingereza.
Akizungumzia sintofahamu hiyo, Sarri anasema kuwa hiyo suala hilo lilikuwa ni kukosekana kwa maelewano tu lakini anatarajia golikipa huyo atajieleza vizuri hali halisi baada ya golikipa kuficha tatizo alilokuwa nalo na kulazimisha kwenda kwenye dakika za nyongeza. Anaamini alikuwa sawa, lakini alitumia njia ambayo siyo sahihi.


Zainabu
Tamaa hiyo jamanii
Furahav
Chelsea hawako vizuri msimu huu.
isha
duuh iyo noma sana
Issa
Sarr anazingua sana