Mechi iliyokuwa ya aina yake kati ya wapinzani wawili wenye vikosi imara, United na Liverpool iliyotawaliwa na ufundi mkubwa na wa aina yake ambapo kila mmoja alikuwa anaangalia namna anavyoweza kuondoka na matokeo ndani ya mchezo huo muhimu sana na wa kusisimua. Walikuwa ni United ambao waliwakaribisha Majogoo katika uwanja wao mgumu kwa mpinzani kuondoka na matokeo.
Pamoja na uzuri wa mechi hiyo ambayo katika kipindi cha kwanza ilionekana kuanza kwa kasi na timu zote kushambuliana; lakini baadaye kuelemea upande mmoja. Japo ilikuwa katika hali hiyo, lakini bado ilionekana kuna ugumu kwa yeyote kupata ushindi ndani ya pambano hilo kubwa baina ya mabingwa hao.
Kilichowashangaza wengi ndani ya mechi hiyo ni vile wachezaji wa Manchester walivyokutana na majeruhi ya aina yake ambapo walilazimika kutumia mbadala wao kipindi cha kwanza pekee cha mchezo huo uliopigwa katika ardhi yao. Wachezaji wote watatu waliweza kuumia dakika za mwanzoni kabisa za mechi hiyo na kumlazimisha mwalimu kufanya mabadiliko ya lazima yasiyokuwa ya kiufundi.
Alikuwa ni Ander Herrera aliyepata majeraha dakika ya 21 tu ya mchezo huo na kufuatiwa mfululizo wa wachezaji wengine wakiwemo Mata na Lingard aliyeingia na kucheza dakika kadhaa tu za mchezo huo na kupata majeraha tena. Jambo hilo lililazimisha kufanya mabadiliko yote ndani ya kipindi kimoja; ambayo kihistoria yalifanywa kwa mara ya mwisho na Newcastle msimu wa 2015.
Ikumbukwe, Lingard aliingia katika kipindi hicho cha kwanza kuchukua nafasi ya mabadiliko ya mchezaji aliyepata majeraha lakini haikumchukua hata dakka nyingi naye aliweza kupata majeraha alipokuwa akigombania mpira na Allison. Akiwa bado hajarudi kwenye ubora wake wa kuuguza majeraha aliyoyapata katika mechi za hivi karibuni ameongeza tena idadi ya majeruhi kikosini hapo.
Mbali na hao pia Matic hakuonekana kabisa katika mchezo huo, kutokana na majeraha aliyoyapata wakati timu hiyo ikiwa katika hatua za mwisho za kujiandaa na mchezo huo ambapo naye ameingia kwenye orodha ya wachezaji ambao United itaendelea kuwakosa. Anaungana na Martial pia ambaye yupo katika hesabu hiyo.
Tathmini yangu
Kwa tathmini ya mchezo United wamecheza mchezo wa kuvutia ambao bila kuangalia aina gani ya wachezaji aliokuwa nao na aina ya kikosi alichokuwa anashindana nacho ndani ya mchezo wake: ni suala ambalo wanastahili pongezi sana. Mabadiliko aliyoyafanya mwalimu kutokana na majeruhi aliokuwa nao ndani ya mechi ile yameleta tija na kuleta njia dhahiri ya kupambana kikosini hapo na kuendana na kasi ya mpinzani wake. Kwa sasa kinachoangaliwa ni mchezo unaofuata na nini kinaweza kutokea ili kurudi katika nafasi yao ya nne ambayo kwa sasa inashikiliwa tena na Arsenal.


Edgar
Asante kwa taarfa
Povel
Don’t miss
Zeiyana
Asante meridianttz kwa taarifa