Nyota wa timu ya Taifa ya Ufaransa Kylian Mbappe ndiye mfungaji bora wa Kombe la Dunia mpaka sasa akiwa amefunga mabao matano na kuongeza mabao manne aliyofunga kwenye kampeni ya Ufaransa ya ushindi wa Kombe la Dunia 2018.

Akiwa tayari amempita Diego Maradona wa Argentina, aliyefunga nane, huku Mreno Cristiano Ronaldo pia akifikisha idadi hiyo. Mbappe ambaye ana umri wa miaka 23, ndiye mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kupachika mabao Kombe la Dunia.
Mbappe amefumania nyavu mara tisa, toka 2018 mpaka sasa akivunja rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na Eusebia wa Ureno aliyetupia nyavuni mara 8 akiwa na miaka 24 na siku 182.

Mchezaji huyo alieisadia Ufaransa kubeba Kombe hilo kwenye kikosi cha Deschamps ni mshambuliaji muhimu sana kutokana na ubora ambao anao hadi sasa kwani licha ya kuwa na uwezo mkubwa wa kupachika mabao anatoa pasi za mabao.
Ufaransa wanatarajia kuvaana na Uingereza katika hatua ya robo fainali ya michuano hii siku ya Jumamosi huku macho mengi ya watu wakiisubiria mechi hii kuona Mabingwa watetezi watafanya nini mwaka huu mbele ya vijana wa Southgate.



