Leeds United Yamtimua Marsch Baada ya Kubamizwa na Nottingham

Klabu ya Leeds United wamemfuta kazi kocha Jesse Marsch kufuatia kichapo cha kusikitisha cha 1-0 hapo jana dhidi ya Nottingham Forest ambao bado wanajitafuta EPL.

 

Leeds United Yamtimua Marsch Baada ya Kubamizwa na Nottingham

Taarifa ya klabu ilisema: “Tungependa kumshukuru Jesse na wafanyakazi wake wa nyuma kwa juhudi zao na tunawatakia heri kwa siku zijazo. Mchakato wa kumteua kocha mkuu mpya unaendelea na tutaendelea kuwajulisha mashabiki katika siku zote zijazo.”

Marsch mwenye miaka 49, amedumu chini ya miezi 12 akiisimamia Elland Road baada ya kuteuliwa kama mrithi wa Marcelo Bielsa mwishoni mwa Februari mwaka jana.

Leeds United Yamtimua Marsch Baada ya Kubamizwa na Nottingham

Kocha huyo raia wa Marekani aliiweka Leeds kwenye Ligi ya Primia msimu wa 2021-22 lakini timu yake imekuwa ikifanya vibaya msimu huu licha ya kuungwa mkono kwa kiasi kikubwa katika soko la uhamisho.

Leeds imesajili wachezaji 10 wapya katika madirisha mawili ya uhamisho ya wachezaji, na watatu waliwasili Januari.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.