Klabu ya Leeds United imefanikiwa kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Marekani na klabu ya Juventus Weston Mckinnie ambaye atakua kwa mkopo klabuni hapo mpaka mwisho wa msimu.
Klabu ya Leeds United chini ya kocha Jesse Marsch wamefanikiwa kumsajili kiungo huyo wa kimarekani ndani ya klabu hiyo ili kuimarisha klabu hiyo kuelekea mwishoni mwa msimu huu, Kwani timu hiyo inaonekana kufanya vizuri msimu huu licha ya kuanza vibaya msimu.
Klabu hiyo imemsajili Weston Mckennie kwa mkopo mpaka mwisho wa msimu huu japo watakua na kipengele ambacho kinaweza kuwaruhusu klabu hiyo kumnunua kwa mkataba wa kudumu ndani ya klabu hiyo kutoka kwa mabingwa zamani wa Italia Juventus.
Klabu ya Juventus ambayo ipo kwenye wakati mgumu baada ya kupokonywa alama 15 ndani ya ligi kuu ya Italia baada ya kukumbwa na kashfa ya matumizi mabaya ya fedha na udanganyifu, Hii ni mara ya tatu wanaachia mchezaji wao kwenda kwa mkopo ligi kuu ya Ungereza kama walivyofanya hapo awali kwa Arthur Mello kujiunga Liverpool,pamoja na Zakaria aliejiunga Chelsea.
Leeds United ya Jesse Marsch inakamata nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza mpaka sasa, Ikiwa ni maendeleo mazuri ndani ya klabu hiyo tofauti na ilivyoanza msimu lakini klabu hiyo inataka kufanya vizuri zaidi na pengine kuweza kumaliza kwenye nafasi za katikati ambazo wanaweza kushiriki michuano ya ulaya na ndio sababu ya kuingia sokoni na kufanya usajili.

