Simeone Asema Hatma yake Itajulikana Mwisho wa Msimu

Kocha wa klabu ya Atletico de Madrid Diego Simeone amesema kua hatma yake juu ya kuendelea kuwepo ndani ya klabu hiyo itajulikana mwishoni mwa msimu huu.

Kocha simeone alizungumza na waandishi wa habari baada ya kipigo walichokipata dhidi ya mahasimu wao klabu ya Real Madrid katika mchezo wa Copa de le Rey juzi alhamisi na kusema kua ataendelea kujitolea ndani ya klabu ya Atletico Madrid, Lakini anaonekana kukataa mazungumzo yake kwasasa.simeoneKlabu ya Atletico Madrid ipo kwenye hali mbaya msimu huu kwani ipo nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu ya Hispania La liga wakiwa nyuma ya vinara Barcelona kwa alama 13 na pia tayari imeshatupw nje katika michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya, Hivo hii inamfanya kocha huyo kua kwenye presha kubwa zaidi.

Kuelekea mchezo wa jumapili wa ligi kuu ya nchini Hispania dhidi ya Osasuna kocha Diego simeone amesema kua mustakabali wake ndani ya klabu ya Atletico de Madrid itafahamika mwishoni mwa msimu huu, Kwani mkataba unategemea zaidi maendeleo ndani ya msimu huu ambavyo yatakua.simeoneKocha huyo ambaye amedumu ndani ya klabu hiyo kwa muda mrefu anaonekana kama amekata tamaa kwasasa pia kwani kwa muda mrefu amekua akipinga suala la yeye kuachana na klabu hiyo kutokana, Lakini wakati huu amekiri hatma yake ndani ya viunga vya Wanda Metropolitano itajulikana mwishoni mwa msimu huu huku akisisitiza bado maamuzi hayapo mkononi mwake ni mkataba ndio utazungumza zaidi.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.