Stefano Pioli Tutakaa Sawa Bila Usajili

Kocha wa klabu ya Ac Milan Stefano Pioli amesema anakiamini kikosi chake ambacho anacho kwasasa hivo haoni haja ya kuingia sokoni katika dirisha la usajili mwezi Januari.

Klabu ya Ac Milan ipo kwenye wakati mgumu baada ya kucheza michezo mitano ndani ya Januari hii lakini hawajafanikiwa kupata ushindi katika mchezo hata mmoja, Huku wakipokea kipigo kizito juzi cha mabao cha mabao manne kutoka kwa Lazio katika mchezo wa ligi kuu ya Italia.stefano pioliKauli ya kocha Stefano Pioli imeshangaza wengi kwani klabu hiyo imekua haina matokeo ya kufurahisha siku za hivi karibuni na ilitarajiwa klabu hiyo kuingia sokoni majira haya ya Januari, Lakini kocha amesema anaamini kikosi chake kinaweza kurejesha makali yake bila kuingia sokoni kuongeza mchezaji yeyote.

Kocha huyo amekiri kua wanapitia kipindi kigumu haswa kiakili lakini yeye anaamini wanaweza kurudisha ubora wao kwa wachezaji haohao waliopo kwenye kikosi, Kwani wachezaji wake wana uwezo na ubora mkubwa ni kuweza kutulia tu na kurejesha hali ya kujiamini ili kuweza kupata matokeo mazuri.stefano pioliKlabu ya Ac Milan haijawahi kucheza michezo sita bila kupata matokeo ikiwa mara ya mwisho ni mwaka 2018 chini ya kocha Gattuso, Kuelekea mchezo wao wa sita wikiendi hii dhidi ya Sassoulo kocha Stefano Pioli anasema watapambana kushinda mchezo huo huenda ukarudisha heshima yao.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.