Winga wa zamani wa Chelsea na Newcastle Christian Atsu ameripotiwa kufukiwa chini ya vifusi vya jengo lililoharibiwa kufuatia tetemeko la ardhi la kipimo cha 7.8 nchini Uturuki. Odds kubwa za soka unazipata Meridianbet.

Zaidi ya watu 1,600 wameuawa na maelfu kujeruhiwa baada ya tetemeko kubwa la ardhi lililoikumba nchi ya Uturuki na Syria usiku wa kuamkia leo.
Kama ilivyoripotiwa na vyombo vingi vya habari nchini Uturuki, operesheni ya kumtafuta na kumwokoa Atsu na majeruhi wengine inaendelea, Christian Atsu alijiunga na klabu ya Ligi Kuu ya Uturuki ya Hatayspor msimu uliopita wa joto.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 alijiunga na Chelsea mwaka 2013 lakini hakuwahi kuichezea klabu hiyo hata dakika moja ya mchezo wa ushindani, kwani alitolewa kwa mkopo kwa klabu kadhaa zikiwemo za Everton na Newcastle.
Ingawa alicheza mechi tano pekee Everton, alivutia vya kutosha kujiunga kwa mkopo huko Newcastle na kuhamia Magpies. Ukiwa na meridianbet unaweza kubashiri mubashara, tembelea maduka ya meridianbet uweze kubashiri.

Kwa jumla aliichezea klabu hiyo mechi 107, akifunga mabao nane, kabla ya kujiunga na Al-Raed ya Saudi mwaka 2021.
Newcastle wamechapisha kwenye mitandao ya kijamii picha ya Christian Atsu alipokuwa katika klabu hiyo, wakisema wanamuombea mema.
Christian Atsu alikuwa uwanjani Jumapili na Hatayspor, akifunga bao dakika ya sabakabla ya mchezo kumalizika katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Kasimpasa. Beti na Meridianbet mechi za ligi zote, odds ni kubwa sana, Usikose hii.
Tetemeko la ardhi lilipiga sana huko Kahramanmaras, ambapo kuna makazi ya wachezaji wa timu ya Hatayspor.
Mchezaji wa Hatayspor Onur Ergun alichapisha hadithi kwenye Instagram kujibu ripoti za awali kwamba habari zilizosambazwa kumhusu yeye sio za kweli.
“Asante sana kwa kila mtu aliyepiga simu na kuuliza,” kiungo huyo alisema. “Habari hizo si za kweli. Niko sawa.
“Siwezi kujibu simu kwa sababu kuna tatizo la mtandao”

