MAPILATO WA SIMBA NA YANGA WAPO TAYARI KWA DABI

Ahmed Arajiga ametangazwa kuwa mwamuzi wa kati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Machi 8 2025 ambapo wababe wawili wanatarajiwa kukutana Yanga na Simba.

MAPILATO WA SIMBA NA YANGA WAPO TAYARI KWA DABI

 

Ikumbukwe kwamba Arajiga alikuwa mwamuzi kwenye mchezo wa Mzizima Dabi uliochezwa Uwanja wa Mkapa baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 2-2 Azam FC wababe hao walipogawana pointi mojamoja baada ya mchezo kukamilika.

Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza ni Ramadhan Kayoko alikuwa ni mwamuzi wa kati ila mzunguko wa pili jina lake halipo kwenye orodha ya waamuzi. Katika mchezo huo baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 0-1 Yanga, bao la Kelvin Kijili aliyejifunga lilidumu mpaka mwisho wa mchezo.

Pia meridianbet inatoa michezo ya kasino ya mtandaoni kama vile, Aviator, poker, Roullette, sloti na mingine kibao. Ingia meridianbet na ucheze sasa.

MAPILATO WA SIMBA NA YANGA WAPO TAYARI KWA DABI

Karim Boimanda Ofisa Habari wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, (TPLB) amesema kuwa kwenye asilimia ya maandalizi wapo juu sana kutokana na kila kitu kuwa kwenye mpangilio mzuri huku akiwataja watakaosimamia mchezo huo.

Salim Singano, Mohamed Mkono, (mwamuzi msaidizi namba moja) hawa kutoka Tanga Kassim Mpanga, (mwamuzi msaidizi namba mbili) kutoka Dar, Amina Kyando,(mwamuzi wa akiba) kutoka Morogoro, Soud Abdi kutoka Dar ikiwa ni baadhi ya maofisa kwenye mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa mwamuzi wa kati atakuwa Ahmed Arajiga.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.