Beki wa Bayer Leverkusen aliye na kiwango cha juu zaidi Piero Hincapie ameongeza mkataba mpya utakaomweka katika klabu hiyo ya Bundesliga hadi 2027 huku Spurs ikimnyemelea.

Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Ecuador amekuwa akifanya vyema tangu kuhama kwake kutoka Talleres ya Argentina kabla ya msimu wa 2021-22 na alihusishwa na kuhamia Tottenham katika dirisha la uhamisho la Januari.
Ana mechi 24 za Kimataifa za Ecuador chini yake, akicheza kila dakika ya mechi tatu za hatua ya makundi ya nchi yake kwenye Kombe la Dunia la Qatar.
Leverkusen wana nia ya kumshikilia mchezaji huyo na wameongeza mkataba wake wa sasa kwa mwaka mmoja ili kuwazuia wawindaji wowote wanaoweza kuwania saini yake.

Hincapie alisema: “Hawakuniahidi sana hapa, lakini kama mchezaji mdogo katika kiwango cha juu walinipa muda wa kucheza niliotaka. Niliweza kujiimarisha hapa na pia kuimarisha nafasi yangu katika timu ya taifa.”
Ni motisha kubwa kwangu kuthibitisha mafanikio yangu katika miaka ijayo na kulenga mataji na Bayer Leverkusen. Alimaliza mchezaji huyo.

