Mshindi mara tano wa medali ya dhahabu katika mashindano ya Paralympic, Ellie Simmonds ametangaza rasmi uamuzi wake wa kustaafu katika mashindano hayo akiwa na miaka 26.

Ellie, 26 alitangaza wiki iliyopita kwamba anatarajia mashindano ya Tokyo 2020 yaliyofanyika Japan kuwa mashindano yake ya nne na mwisho kushiriki fainali za michuano ya Paralympic.
Ellie alichaguliwa mmoja kati ya mchezaji bora kupeperusha bendera za Britain katika ufunguzi wa michuano hiyo ya Paralympic huko Japan, alipanga kurudi nyumbani na kutathmini kazi yake na sasa ameamua ni wakati wa kutundika miwani.
Ellie Simmonds alijitambulisha kama mmoja wa Paralympian anayejulikana zaidi wa Britain kwa kushinda dhahabu mara mbili huko Beijing mwaka 2008 akiwa na umri wa miaka 13 na kushinda dhahabu mbili zaidi huko London miaka minne baadaye.
Alishinda dhahabu tena huko Rio 2016 lakini alishindwa kutwaa tena huko Tokyo.
Simmonds alimaliza wa tano katika mbio zake za mwisho za kuogelea, Alhamisi iliyopita ya S6 400m freestyle – baada ya kutoridhishwa kwa awali kuondolewa kwa rufaa.

Meridianbet inakuletea ushindi kwenye kiganjani kwako, unafurahia radha halisi ya burudani ya kasino mtandaoni na tabasamu la ushindi.


