Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amehaidi kudhamini Mashindano ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kwa upande wa wanawake.

Rais Samia ametoa ahadi hiyo siku Jumapili alipokuwa anatoa hotuba kwenye hafla ya kukabidhiwa kombe la CECAFA kwa wanaume lilibebwa na timu ya U20 pamoja na kuwapongeza wanamichezo waliofanya vizuri kwenye Olimpiki 2021.
Mama Samia alisema Rais wa TFF Wallace Karia ndiye ambaye alimshawishi na kumwambia kuwa aige kile anachofanya Rais Paul Kagame wa Rwanda ambaye anadhamini CECAFA ya wanaume na akampa bajeti ambayo aliikubali.
“Kuna ombi nilinong’ona na Rais wa TFF, aliniambia anataka kuanzisha mashindano ya CECAFA Women Championship na yanataka udhamini, akanishawishi kwa kusema mwenzako Kagame anadhamini mashindano fulani na wewe utadhamini haya.
Nikamwambia nitajie kiasi ili nitazame misuli yangu, akanitajia hicho kiasi ambacho sitakitaja hapa, nikapima misuli yangu nikasema sitoweza ila nitajua nitakakozipata, kwahiyo niwatangazie kuwa nitadhamini hayo mashindano.”
Unawezaje kuikosa hii! Ndani ya kasino za meridianbet kuna mchezo unaoweza kukupa mkwanja mrefu leo hii, Wild Hot 40 ni njia nyingine ya kukufanya milionea, Chagua namba yako na uvune mkwanja.



Sarah
Safi