Roma wanawasiliana kwa karibu na Celta Vigo huku wakitafuta kushindana na Wolves kwa Jorgen Strand Larsen na pia wameelekeza macho yao kwa Albert Gudmundsson wa Genoa.

Mradi mpya wa Giallorossi unaanza kuimarika chini ya kocha Daniele De Rossi, ambaye hivi majuzi alisinya kandarasi ya miaka mitatu na klabu hiyo. Sasa ana kazi ngumu ya kupanga dirisha la uhamisho la klabu katika majira ya joto pamoja na mkurugenzi wa michezo Florent Ghisolfi.
Roma tayari wamemuuza Andrea Belotti kwenda Como kwa takriban €4.5m na wanatafuta kumsafirisha Houssem Aouar hadi Mashariki ya Kati kwa ada ya karibu €8-10m. Pia wamo Rick Karsdorp, Chris Smalling, Zeki Celik, Edoardo Bove na Nicola Zalewski.


