Cristiano Ronaldo alifunga bao lake la kwanza kwa Al Nassr na kuipatia timu yake pointi moja dhidi ya Al Fateh siku ya jana.

Nahodha huyo wa Ureno, ambaye alihamia Saudi Arabia kama mchezaji huru alifungua akaunti yake kwa kupachika bao la penalti ya dakika za lala salama katika Uwanja wa Prince Abdullah bin Jalawi.
Vinara hao wa Saudi Pro League Al Nassr walitoka nyuma mara mbili na kupata pointi moja ugenini.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 37 alipiga mkwaju wake kwa utulivu dakika ya 92 kabla ya mchezaji mwenzake Talisca, ambaye alifunga bao la kwanza la Al Nassr kufuta bao la kuongoza la Cristian Tello, kutolewa nje kwa kadi nyekundu katika mchezo wa mwisho.

Ronaldo alikuwa ameifungia Riyadh All-Stars mabao mawili katika sare ya 5-4 ya kirafiki dhidi ya Paris Saint-Germain iliyojumuisha Lionel Messi na Kylian Mbappe mwezi uliopita.

