Mchezaji wa zamani wa Manchester United, Wyne Rooney amesema mshambuliaji mwezake wa zamani aliyerejea klabuni hapo ana uwezo wa kuendelea kusakata kabumbu mpaka umri wa miaka 40.

Ronaldo, 36, alikaa misimu sita Old Trafford kati ya 2003 na 2009, akishinda mataji manane makubwa, na sasa amejiunga tena na United kutoka Juventus mwezi uliopita kwa kandarasi ya miaka miwili.
“Mara ya mwisho kucheza hapa, alikuwa mkimbiaji zaidi, mpiga chenga mzuri, kwa kasi na nguvu,” alisema Rooney, ambaye sasa anakinoa kikosi cha Derby Contry.
“Kwa sasa ni mfungaji. Nadhani mchezo wake umebadilika sana.”
Rooney, ambaye ni mfungaji bora wa muda wote wa Manchester United, amesema kwasasa Ronaldo ni mchezaji tofauti kabisa na yule aliyeondoka klabuni hapo miaka 12 iliyopita lakini bado anaweza kumudu mahitaji ya Ligi Kuu.
“Uwezo wake ni jambo moja, lakini basi pia anajitunza sana, bado yuko katika hali nzuri. Haitanishangaza ikiwa anacheza hadi ana miaka 40, kama Ryan Giggs, na bado anafunga mabao.
“Wachezaji wenzake watalazimika kufanya kazi kwa bidii kidogo. Lakini kama itakuwa kama miaka miwili ya mwisho niliocheza naye, timu ilimruhusu kufanya hivyo kwa sababu anafunga magoli, na magoli yanakupa ushindi wa mchezo. ” aliongeza Rooney
Ronaldo, ambaye aliifungia Manchester United mabao 118 wakati wa kipindi chake cha kwanza, anatarajiwa kucheza watakapomenyana na Newcastle kwenye Ligi ya Premia Jumamosi hii.
Meridianbet inakuletea ushindi kwenye kiganjani kwako, unafurahia radha halisi ya burudani ya kasino mtandaoni na tabasamu la ushindi.


