Shaqiri Kutua Lyon kwa £9.5m.

 

Klabu ya Liverpool imekubali dau la £9.5m kutoka Lyon kwaajili ya kumuuza kiungo mshambuliaji wa Uswis, Xherdan Shaqiri baada ya kushindwa kukubaliana mwezi januari.

 

Klabu hizo zimekubaliana ada kwa mchezaji huyo wa miaka 29 na Lyon alithibitisha Jumapili kwamba atafanya vipimo vya afya leo [Jumatatu] kabla ya kukamilisha uhamisho huo.

Shaqiri ameshakubaliana maslahi binafsi na Lyon na taarifa zinasema atasaini mkataba wa miaka minne mpaka mwaka 2025.

“Olympique Lyonnais inafurahi kuwa hatimaye imefikia makubaliano na Liverpool kwa uhamisho wa kiungo wa kimataifa wa Uswizi, Xherdan Shaqiri,” ilisema taarifa kwenye website ya Lyon.

 

“Shaqiri, ambaye amevutiwa na project ya OL, atawasili Lyon usiku wa leo [jana] ambapo atakaribishwa na Juninho. Kukamilisha uhamisho huo kunabaki kwa vipimo vya afya ambao mchezaji atafaulu Jumatatu hii asubuhi na kukamilika kwa taratibu za mwisho za kiutawala.”

Shaqiri aliweka wazi nia yake ya kuondoka Liverpool msimu huu wa joto kutafuta nafasi ya kucheza. Anaondoka akiwa amecheza mechi 63 kwa klabu tangu ajiunge kutoka Stoke mnamo 2018, na kutwaa Ligi ya Mabingwa, UEFA Super Cup, FIFA Club World Cup na Ligi Kuu EPL.


NAMBA 40 ZA MKWANJA

Unawezaje kuikosa hii! Ndani ya kasino za meridianbet kuna mchezo unaoweza kukupa mkwanja mrefu leo hii, Wild Hot 40 ni njia nyingine ya kukufanya milionea, Chagua namba yako na uvune mkwanja.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe