Simba SC Kuendelea Kutangaza VISIT TANZANIA.

 

Klabu ya Simba SC itaendelea kutangaza utalii katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika kama tulivyofanya msimu uliopita kwenye Ligi ya Mabingwa.

 

Simba SC Kuendelea Kutangaza VISIT TANZANIA.

 

Katika mechi za Kombe la Shirikisho kuanzia Jumapili dhidi ya ASEC Mimosas kutoka Ivory Coast wachezaji wa Simba SC watavaa jezi zilizoandikwa VISIT TANZANIA kifuani.

Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba SC, Barbara Gonzalez amesema kwa sasa timu inatambulika vizuri Afrika kuliko wengi wanavyodhani ndiyo maana Bodi ya Utalii imeona ni vema kuendelea kutangaza.

“Simba inaheshimika sana Afrika kuliko inavyochukuliwa hapa nchini, Simba inaongoza kwa kuingiza mashabiki wengi Afrika hiyo ni heshima kubwa. Brand ya Simba imezidi kuwa kubwa na hii inatufanya kuendelea kutangaza utalii.

“Katika mechi zetu zote za Kombe la Shirikisho tutaavaa jezi zilizoandikwa VISIT TANZANIA kifuani kuendelea kutangaza Utalii kama ilivyokuwa msimu uliopita. Jezi mpya kwa ajili ya michuano hii zitaanza kuuzwa kesho [leo] kwenye maduka ya Vunjabei,” amesema Barbara.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii, Jaji Thomas Mihayo amesema takwimu zinaonyesha idadi ya watalii wa ndani na Afrika imeongezeka kitu ambacho Simba imechangia kwa kiasi kikubwa.

Simba ni Mabalozi wetu wa Kimataifa ndiyo maana watavaa jezi zilizoandikwa Visit Tanzania kama ilivyokuwa mwaka jana. Kupitia michezo Wananchi wameanza kuhamasika na Watanzania wamekuwa wakiongezeka katika mbuga zetu wakifuatiwa na wageni kutoka Afrika. Mchango wa Simba ni mkubwa katika Utalii,” amesema Jaji Mihayo.


KASINO YA MTANDAONI: EMOTICOINS SABABU YA KUVUNA ZAIDI.

Haijawahi kuwa rahisi hivi kwenye safari yako ya kuvuna mkwanja, kasino maridhawa ya meridianbettz inakuletea mchezo wa Emoticoins unaokupa nafasi ya kufanya safari yako kuwa rahisi zaidi. Wakati ni wako nafasi ni yako na Emoticoins.

senegal, Senegal Mabingwa AFCON 2021., Meridianbet

CHEZA HAPA.

Acha ujumbe