Oblak Hakukumbuka Mengi Yaliyotokea Baada ya Kupata Hitilafu Kidogo

Kipa wa Atletico Madrid Jan Oblak hakukumbuka kilichotokea na atawekwa chini ya uangalizi baada ya “kuchanganyikiwa kidogo” katika ushindi wa 1-0 wa hapo jana kwenye LaLiga dhidi ya Athletic Bilbao.

 

Oblak Hakukumbuka Mengi Yaliyotokea Baada ya Kupata Hitilafu Kidogo

Oblak alitolewa nje katika dakika ya 69 kama sehemu ya mabadiliko matatu kutokana na tatizo la bega, huku mbadala wake Ivo Grbic akiokoa dakika za mwisho huko San Mames.

Atletico walithibitisha hilo  baada ya mchezo huo kwamba mlinda mlango huyo wa Slovakia alitolewa kwa sababu alikuwa amechanganyikiwa kidogo, pia alipata majeraha ya moja kwa moja kwenye bega lake la kulia.

Kocha mkuu wa Atletico Diego Simeone aliongeza kwa kusema kuwa; “Jan hakukumbuka mengi ya kilichotokea sijazungumza naye, lakini daktari aliniambia kuwa hakumbuki.”

Klabu hiyo ilisema Oblak alifanyiwa uchunguzi wa mishipa ya fahamu baada ya mchezo bila dalili zozote za wasiwasi, lakini atawekwa chini ya uangalizi wa madaktari.  Oblak alijaribu kucheza baada ya kuonekana akiuguza jeraha la bega kabla ya kuzimia katika dakika ya 69.

Oblak Hakukumbuka Mengi Yaliyotokea Baada ya Kupata Hitilafu Kidogo

Mlinda mlango huyo ameanza mechi nane kati ya tisa za ligi ya Atletico msimu huu, baada ya kusumbuliwa na tatizo la paja mapema Septemba.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.