Southampton Yamtimua Kocha wao Jones

Nathan Jones amefukuzwa kazi kama kocha mkuu wa Southampton baada ya mechi 14 pekee ambazo amezisimamia baada ya kuteuliwa.

 

Southampton Yamtimua Kocha wao Jones

Jones mwenye miaka 49, alichukua jukumu la St Mary’s Novemba mwaka jana, akichukua nafasi ya kocha wa zamani Ralph Hasenhuttl.

Kocha huyo wa Wales anaiacha Saints kwenye nafasi ya mwisho, pointi nne kutoka kwenye usalama, baada ya kupoteza mechi tisa kati ya 10 za mwisho za ligi kutokana na kichapo cha 2-1 jana kutoka kwa Wolves.

Taarifa ya klabu ilithibitisha: “Klabu ya soka ya Southampton inaweza kuthibitisha kuwa imeachana na meneja wa kikosi cha kwanza cha wanaume Nathan Jones.”

Southampton Yamtimua Kocha wao Jones

Makocha wa kikosi cha kwanza Chris Cohen na Alan Sheehan pia wameondoka kwenye klabu. Kocha mkuu wa kikosi cha kwanza Ruben Selles atachukua jukumu la mazoezi na kuandaa timu kabla ya mchezo wa wikendi ijayo dhidi ya Chelsea.

Southampton watawatembelea Chelsea Jumamosi na wapinzani wao walioshuka daraja Leeds wikendi ifuatayo katika mchuano muhimu.

Southampton Yamtimua Kocha wao Jones

Steven Gerrard, Marcelo Gallardo, Jesse Marsch na Mauricio Pochettino wanaaminika kuwa miongoni mwa wagombea wa mapema kuchukua nafasi hiyo kwa kudumu.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.