Toni Kroos Bado Hajaamua Kuongeza Mkataba Madrid

Kiungo wa klabu ya Real Madrid Toni Kroos inaelezwa kua hajafikiria kuongeza mkataba mpya ambao utaendelea kumbakiza ndani ya klabu hiyo ambayo ameitumikia kwa muda mrefu.

Kiungo Toni Kroos ambaye amekua kwenye kikosi cha Real Madrid ambacho kimefanikiwa kutwaa ubingwa wa tano wa klabu bingwa ya dunia baada ya kuifunga klabu ya Al-Hilal kwa mabao matano kwa matatu. Kiungo huyo anazungumzwa kua kwenye mazungumzo na klabu yake kwajili ya kuongeza mkataba wake.Toni KroosKlabu ya Real Madrid imekua kwenye mazungumzo na kiungo huyo wa Kijerumani kwajili ya kuongeza mkataba mpya wa kuendelea kusalia ndani ya klabu hiyo, Mkataba wa kiungo huyo fundi unatamatika mwiisho wa msimu huu hivo klabu hiyo inahitaji kumbakiza ndani ya klabu hiyo.

Toni Kroos amezungumzwa mara kadhaa kua anahitaji kustaafu soka ndani ya klabu hiyo na yeye mwenyewe akithibitisha hilo, Hivo ni jambo ambalo linaonesha kua kiungo anaweza kusaini mkataba mpya ndani ya timu hiyo au huenda akastaafu mwishoni mwa msimu huu vilevile ndani ya klabu hiyo.Toni KroosKlabu ya Real Madrid ipo kwenye mchakato wa kuwaongezea mikataba baadhi ya magwiji wake ndani ya klabu hiyo wakifanikiwa kuwashawishi wachezaji kama Karim Benzema na Luca Modric ambao tayari wamekubali kusaini mkataba mpya ndani ya timu hiyo, Lakini Toni Kroos haijafahamika ni lini atakubali kusaini mkataba mpya klabuni hapo.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.